Utafiti: Karibu wanawake 200 waliuawa Kenya mwaka 2024
27 Januari 2025Ripoti ya kila mwaka ya kundi linalopambana na vitendo vya kuwanyamazisha wanawake kwa ushirikiano na kampuni ya data ya Odipo Dev pamoja na chombo cha habari cha Africa Uncensored, iligundua kuwa wanawake 170 waliuawa mwaka jana, kutoka 95 mwaka uliopita.
Soma pia:Rais wa Kenya William Ruto akiri ukiukaji wa polisi katika maandamano
Mtafiti mkuu wa kundi hilo Patricia Andago amesema mwaka 2024 ulikuwa mwaka mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa wanawake wa Kenya, na kwa bahati mbaya hakuna dalili zozote zinazoashiria kuwa vitendo hivyo vitapungua.
Suala la unyanyasaji wa kijinsia limeenea katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, ambapo mwaka jana, polisi waliwafyetulia mabomu ya machozi wanaharakati walipojaribu kuandamana katika mji mkuu wa Nairobi wakitaka kukomeshwa kwa mauaji ya wanawake.