Ushuru wa Trump waanza kutekelezwa
9 Aprili 2025Matangazo
Hatua hii imetikisa utaratibu wa biashara kimataifa na kuvuruga masoko ya hisa. Trump ametoa ishara tofauti kwa wawekezaji kwamba huenda ushuru huo utabaki kwa muda mrefu, lakini pia akijigamba kuwa hatua hiyo imeshinikiza viongozi kuomba mazungumzo.
Utawala wa Trump umepanga mazungumzo na Korea Kusini na Japan, washirika wake wa karibu kibiashara, huku Waziri Mkuu wa Italia Giorga Meloni akitarajiwa kuzuru Washington wiki ijayo.
Soma pia: Umoja wa Ulaya uko tayari kuingia kwenye mazungumzo na Marekani kuhusu ushuru
Hata hivyo China kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya nje Lin Jian, imeapa kuchukua hatua madhubuti ili kulinda maslahi ya taifa hilo.