Ushuru mpya dhidi ya Canada na China waanza kutekelezwa
4 Machi 2025Wakati huo huo, Trump amesaini agizo la kuongeza ushuru zaidi kwenye bidhaa za China.
Akizungumzia hatua hiyo Lin Jian, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema, "Ningependa kurudia kwamba watu wa China hawatatishika. Haturuhusu kamwe kuonewa. Shinikizo, kulazimishwa na vitisho sio njia sahihi ya kukabiliana na China."
Soma pia: Trump asema Canada na Mexico haziwezi kuzuia ushuru
Awali, Trump alikuwa ametangaza ushuru wa asilimia 10 na sasa ameongeza maradufu, hadi asilimia 20 kwenye bidhaa mbalimbali za kutoka China.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, amesema kuwa hakuna uhalali wa ushuru huo uliotangazwa na Trump. Amesema Canada itaanzisha Jumanne ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani ili kulipiza kisasi ushuru wa Marekani.