Tanzania imekuwa ikifanya utafiti kuhusu ugunduzi wa gesi asilia kwa zaidi ya miaka hamsini, na ugunduzi wa kwanza ulifanyika mwaka 1974 katika kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi na baadaye mkoani Mtwara. Lakini usalama wa miundombinu ya gesi na changamoto zake kwa mazingira ni zipi?