Usafiri wa reli warejea kawaida baada ya shambulio Hamburg
24 Mei 2025Matangazo
Shambulio hilo lililotokea Ijumaa (23.05.2025) jioni, kwenye kituo kikuu cha treni, lilisababisha operesheni kubwa ya polisi na waokoaji. Wachunguzi walikuwa na shughuli nyingi kupata ushahidi hadi usiku.
Polisi walimkamata mshukiwa ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 39 katika eneo la tukio, na kusema atafikishwa mbele ya hakimu baadaye leo Jumamosi.
Wachunguzi kwa sasa wanaamini kuwa kisa hicho kilietendwa na mtu mmoja pekee na bado hakuna ushahidi wa tukio hilo na mafungamano yoyote ya kisiasa.