MigogoroUlaya
Urusi: Nchi za Ulaya zinalenga "kuzuia" mchakato wa amani
24 Agosti 2025Matangazo
Lavrov amekemea hatua ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ya kuweka masharti na kulazimisha kukutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, akisisitiza kuwa majaribio hayo yanalenga kuvuruga mchakato wa amani ulioanzishwa na marais Trump na Putin, ambao umeonyesha matokeo mazuri.
Kauli ya Lavrov imetolewa wakati Urusi ikiilaumu pia Ukraine kwa kushambulia kinu cha nyuklia katika mji wa mpakani wa Kursk lakini shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA limesema hakuna hatari yoyote ya mionzi. Hayo yanajiri wakati leo Ukraine imekuwa ikiadhimisha miaka 34 tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Umoja wa Kisovieti.