Urusi yauwa watu 13 Ukraine
26 Mei 2025Matangazo
Maafisa wa Ukraine wameyaelezea mashambulizi hayo ya anga kuwa makubwa na ya pili mfululizo, yakijumuisha mji mkuu, Kiev.
Kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine, waliouawa ni pamoja na watoto wenye umri wa miaka minane, 12 na 17 katika jimbo la kaskazini magharibi la Zhytomyr.
Soma zaidi: Urusi yafanya mashambulizi katika mji wa Lviv,Ukraine na kuuwa watu 7
Rais Volodymyr Zelensky amesema kimya cha Marekani na washirika wake kinampa Rais Vladimir Putin wa Urusi hamasa ya kuongeza mashambulizi.
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, ametaka shinikizo kubwa la kimataifa dhidi ya Urusi ili kukomesha vita hivyo.