Urusi yathibitisha nia ya mazungumzo na Ukraine
21 Julai 2025Matangazo
Hii leo, msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov, amesema kuwa katika mikutano ya awali, pande zote mbili zilibadilishana misimamo yao iliyoandikwa kwenye nyaraka .
Urusi: Tunatafari pendekezo la mazungumzo ya amani
Kwa Urusi: Tunatafari pendekezo la mazungumzo ya amanimujibu wa vyombo vya habari vya Urusi, Peskov amesema kubadilishana mawazo na mazungumzo bado hakujatekelezwa lakini kufikia sasa wanapinga kikamilifu.
Peskov ameongeza kuwa juhudi kubwa za kidiplomasia bado zinahitajika.
Siku ya Jumamosi, Zelensky alipendekeza mkutano ufanyike baadaye wiki hii. Kulingana na Peskov, hakuna tarehe iliyopangwa. Alisema hakuna mabadiliko kwa upande wa Urusi kuhusu atakayejumuishwa kwenye ujumbe wa mazungumzo.