Urusi yateka maeneo mawili zaidi mashariki mwa Ukraine
6 Julai 2025Matangazo
Ukraine haijatoa tamko rasmi kuhusu madai hayo ya Moscow.Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, Urusi imekuwa ikisonga taratibu katika mstari wa mbele, ikitumia faida yake dhidi ya wanajeshi wa Ukraine waliodhoofika kwa idadi na rasilimali.Kijiji cha Piddubne, kilichokuwa na wakazi takriban 500 kabla ya vita, kiko umbali wa kilomita saba kutoka mpaka wa mkoa wa Dnipropetrovsk, wakati Sobolivka kiko karibu na mji wa Kupiansk.Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, wanajeshi wao wameyakomboa maeneo hayo, iliyoyataja kwa kutumia tahajia za Kirusi. Ripoti ya taasisi ya utafiti wa vitia ya Marekani, ISW, inaonyesha kuwa mafanikio ya Urusi mwezi Juni yalikuwa makubwa zaidi tangu Novemba mwaka jana.