Ahadi ya kusitishwa mapigano Pasaka Ukraine yavunjika
20 Aprili 2025Matangazo
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vya Ukraine vilijaribu kushambulia vijiji vya Urusi vya Sukhaya Balka na Bogatyr vilivyoko katika mkoa wa mashariki wa Donetsk lakini yalizimwa. Wanajeshi wa Ukraine walijaribu pia kushambulia miji mingine kadhaa ya Urusi ikiwemo Kursk,kwa mujibu wa Urusi. Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky alisema nchi yake itaheshimu tangazo la rais Putin la kusitisha vita kupisha Pasaka, lakini vikosi vyake vitajibu ikiwa ahadi hiyo itakiukwa.Zelensky leo amesema Urusi bado inaendelea kuishambulia nchi yake.