Urusi yarusha droni zipatazo 151 kuishambulia Ukraine
9 Februari 2025Matangazo
Ukraine imeserma jeshi lake la anga lilifanikiwa kuzidungua ndege 70 zisizo na rubani, na kwamba 74 hazikufanikiwa kufikia malengo yake kutokana na jeshi la Ukraine kuzivuruga kwa njia za kielektroniki. Wakati huo huo shirika la Habari la Urusi TASS, limeripoti kwa kuinukuu wizara ya ulinzi ya Urusi kwamba wanajeshi wake wameudhibiti mji wa Orikhovo-Vasylivka wa mashariki mwa Ukraine katika mkoa wa Donetsk.