Urusi yaridhishwa na mazungumzo ya kusitisha vita Ukraine
25 Machi 2025Matangazo
Mjumbe wa Urusi Grigory Karasin amenukuliwa leo na shirika la habari la serikali ya nchini hiyo TASS akisema kwamba kwa ujumla, hamu bado iko ya kufanyika kwa mazungumzo ya tija yanayohitajika.
Karasin amesema mazungumzo yaliofanywa Riyadh jana Jumatatu yataendelezwa, na akaongeza kuwa mataifa mengine pamoja na Umoja wa Mataifa pia yatashirikishwa lakini hakutoa maelezo zaidi.
Wakati huo huo, maafisa wa Ukraine na Marekani wanatarajiwa kufanya mazungumzo mengine leo mjini Riyadh. Haya ni kulingana na chanzo cha Ukraine.
Mjumbe mmoja wa Ukraine katika mazungumzo hayo, amewaambia waandishi wa habari kwamba bado wanashirikiana na maafisa wa Marekani.