SiasaUrusi
Urusi yapinga pendekezo la mazungumzo kufanyika Vatican
23 Mei 2025Matangazo
Sergei Lavrov ametoa kauli hiyo baada ya rais wa Marekani Donald Trump kupendekeza, wakati wa mazungumzo yake kwa njia ya simu na rais Vladimir Putin wa Urusi, kuwa mji wa Vatican ni mahala pa kufanyaia mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine.
Pendekezo hilo haliungwi mkono na wengi nchini Urusi. Hadi sasa haijulikani ni wapi au lini mazungumzo ya moja kwa moja baina ya Urusi na Ukraine yatafanyika.
Kulingana na vyanzo vya ndani nchini Urusi, ni kwamba Moscow inaendelea kuifanyia kazi rasimu yake ya mapendekezo ya kutatua mzozo huo.