Urusi yapatikana na hatia ya ukiukaji wa haki Ukraine
9 Julai 2025Matangazo
Akisoma uamuzi huo mjini Strasbourg mbele ya mahakama iliyojaa watu, Jaji Mattias Guyomar alisema vikosi vya Urusi vilikiuka sheria ya kimataifa ya kibinadamu kwa kufanya mashambulizi yaliyosababisha vifo na majeraha kwa maelfu ya raia, na kueneza hofu kwa makusudi.
Russia, USA, zakubaliana kufikisha mwisho vita Ukraine
Majaji walibainisha kuwa mashambulizi hayo yalizidi mipaka ya malengo ya kijeshi, huku ukatili wa kingono ukitajwa kutumika kama mbinu ya kuvunja morali ya upande wa Ukraine.
Madai mengine yaliyotolewa dhidi ya Urusi ni pamoja na mateso, ubakaji, uharibifu wa miundombinu ya kiraia, na utekaji nyara wa watoto wa Kiukreni.