Urusi yakataa kupangiwa na EU kusitisha vita Ukraine
12 Mei 2025Matangazo
Urusi imesema haiwezi kukubali kupewa muda wa mwisho na Umoja wa Ulaya kusitisha vita nchini Ukraine.
Tamko hilo la Kremlin limetolewa baada ya viongozi wa Umoja wa Ulaya kuitaka Urusi ikubali,kufikia leo usiku, pendekezo la kusitisha vita kwa siku 30.Soma pia: Viongozi wa Ulaya wakutana London kuujadili mzozo wa Ukraine
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka Ufaransa,Italia,Ujerumani,Uhispania, Poland na Umoja wa Ulaya wanakutana mjini London na mwenyeji wao David Lammy,waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, kujadili hatua za kuchukuwa dhidi ya Urusi.
Lammy anatarajiwa kutangaza vikwazo zaidi vitakavyowalenga washirika wa Urusi.