Urusi yakaribisha hatua ya Marekani kupunguza silaha Ukraine
2 Julai 2025Shirika la habari la Urusi Interfax limeripoti kuwa msemaji wa Ikulu Dmitry Peskov amesema hatua ya Ukraine kupokea silaha chache za kijeshi inatoa nafasi ya kufikia tamati operesheni ya Moscow nchini humo.
Urusi mara zote imekuwa ikiuita uvamizi na uchokozi wake dhidi ya Ukraine kama operesheni maalum ya kijeshi.
Guterres aahidi msaada wa kuijenga upya Ukraine
Marekani imesema ilitangaza kwamba haitoendelea kutoa silaha zilizoahidiwa zamani na taifa hilo kwa Ukraine kufuatia wasiwasi uliopo katika hifadhi yake. Silaha ambazo hazitosafirishwa tena kuelekea Ukraine zinajumuisha mifumo ya ulinzi wa anga.
Ukraine kupitia wizara yake ya ulinzi imeomba ufafanuzi juu ya hatua ya Marekani ikisema haikufahamishwa kuhusu kupunguzwa kwa usaidizi huo wa kijeshi. Hata hivyo Umoja wa Ulaya inaendelea kutoa silaha kwa Ukraine na unaisaidia nchi hiyo kutanua utengenezaji wa silaha zake. Ujerumani kwa mfano inafadhili mpango wa Ukraine wa kutengeneza makombora.