MigogoroUkraine
Urusi yaishambulia Kyiv kwa mabomu na droni
24 Mei 2025Matangazo
Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi ilirusha makombora 14 ya masafa marefu na droni 250 usiku wa kuamkia leo, na kuongeza kuwa lilidungua makombora sita na droni 245.
Maafisa pia wamesema raia watano wameuawa kwa mashambulizi ya Urusi katika mikoa ya Kharkiv na Donetsk. Wakati huo huo jeshi la Urusi lilisema kuwa Ukraine iliilenga Urusi kwa droni na makombora 788 tangu Jumanne.
Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky amelaani vikali mashambulizi hayo na kutoa wito wa vikwazo zaidi vya kimataifa dhidi ya Urusi.