Urusi yaishambulia Kharkiv kwa usiku wa pili mfululizo
31 Machi 2025Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa Telegram, meya wa Kharkiv Ihor Terekhov, amesema shambulizi hilo dhidi ya Kharkiv, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, lilifanyika kwa muda mrefu katika saa za usiku na kulenga wilaya kubwa na kongwe zaidi.
Watu watatu wauawa Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi
Trekhov ameongeza kuwa wafanyakazi wa dharura wamesema walipambana na moto mkubwa ulioenea umbali wa mita za mraba 3,900 baada ya shambulizi hilo.
Jeshi la anga la Ukraine ladungua droni 57 za Urusi
Jeshi la anga la Ukraine limesema limedungua droni 57 kati ya 131 zilizorushwa na Urusiwakati wa shambulizi hilo la usiku ambalo pia lilitumia makombora mawili aina ya Iskander-M .
Jeshi hilo limeongeza kusema droni nyingine 45 hazikufikia shabaha zake kutokana na hatua za kinga za kielektroniki.