Urusi yahusishwa na shambulizi la GPS kwenye ndege ya Leyen
1 Septemba 2025Urusi inashutumiwa kuhusika na tukio la kuzimika ghafla kwa mfumo wa GPS wa ndege iliyokuwa imembeba Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wakati ikiwa angani kuelekea Bulgaria jana Jumapili.
Msemaji wa Halmashauri hiyo Arianna Podesta amewaambia waandishi wa habari kwamba mamlaka ya Bulgaria zinaamini Moscow imehusika na kisa hicho cha jana, ingawa haiko wazi ikiwa ndege ililengwa kwa makusudi kwa kuwa ni kawaida mashambulizi kama hayo kufanyika kwenye eneo hilo.
Hata hivyo ndege hiyo ilitua salama kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Plovdiv, kusini mwa Bulgaria, bila ya kulazimika kubadilisha njia.
Von der Leyen alikwenda Bulgaria ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye mataifa saba ya mashariki mwa Ulaya yanayopakana na Urusi na ambayo yanakabiliwa zaidi na vitisho vya kila wakati kutoka Moscow.