MigogoroUlaya
Urusi yaharibu miundombinu ya umeme kusini mwa Ukraine
7 Machi 2025Matangazo
Hayo yameelezwa na Gavana wa mji huyo Oleh Kiper kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram. Amesema kwenye viunga nje kidogo ya mji wa Odesa, nyumba tatu za watu binafsi zimewaka moto na miundombinu ya umeme imeharibiwa.
Mashambulizi ya droni za Urusi yameutikisa mji huo karibu kila siku ndani ya wiki hii. Hapo Jumatano usiku, watu wawili walijeruhiwa huku mtu mmoja alikufa siku ya Jumanne baada ya kuangukiwa na mabaki ya makombora.
Uharibifu wa vituo vya kufua au kusambaza umeme umepelekea kukosekana nishati hiyo muhimu pamoja na huduma za maji au vipasha joto majumbani.