Urusi yafanya shambulizi kubwa zaidi la droni nchini Ukraine
9 Julai 2025Matangazo
Jeshi la Ukraine limesema Urusi ilirusha droni 728 na makombora 13, huku mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine ikifanikiwa kunasa droni 711 na kudungua takriban saba kati ya makombora hayo.
Watu watatu wauawa Urusi kwa shambulio la Ukraine
Kupitia chapisho kwenye mitandao ya kijamii, Rais Volodymyr Zelensky amesema mashambulizi hayo si ya kawaida, bali ni ujumbe wa kisiasa unaokuja wakati ambapo kuna jitihada nyingi za kidiplomasia za kufanikisha usitishaji wa mapigano na kurejesha amani.
Zelensky ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza vikwazo dhidi ya Urusi, hasa katika sekta ya nishati ambayo, kulingana naye, inaendelea kuiingizia Moscow mapato yanayotumiwa kufadhili vita.