Urusi yafanya shambulizi kubwa zaidi la anga dhidi Ukraine
7 Septemba 2025Matangazo
Msemaji wa jeshi la anga Yuriy Ihnat amethibitisha kuwa jumla ya droni 805 na makombora 13 yalirushwa, huku vikosi vya Ukraine vikiangusha droni 747 na makombora manne. Mengine yaliangukia maeneo manane nchini humo, na mashambulizi ya moja kwa moja yalirekodiwa katika majengo ya makazi jijini Kyiv.
Waziri Mkuu Yulia Svyrydenko amesema dunia lazima ijibu mashambulizi hayo kwa vitendo, sio maneno pekee, ikiwa ni pamoja na kuimarisha vikwazo dhidi ya mafuta na gesi ya Urusi.
Shambulio hili ni la pili kubwa kuilenga Kyiv ndani ya wiki mbili, wakati matarajio ya mazungumzo ya amani yakizidi kufifia.