MigogoroUlaya
Urusi yaishambulia Ukraine kwa droni 88
12 Aprili 2025Matangazo
Watu wanne wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo. Meya wa mji mkuu Kyiv, Vitali Klitchko amebainisha kuwa watu watatu wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo.
Soma zaidi: Mashambulizi ya droni na Makombora yashuhudiwa Kyiv, Urusi yadungua droni za Ukraine
Mabaki ya droni zilizodunguliwa yameiharibu nyumba moja binafsi, majengo kadhaa ya biashara na kusababisha moto mkubwa kwenye maeneo kadhaa ya mji huo mkuu wa Ukraine.
Katika mji wa Kharkiv, meya Ihor Terekhov ameripoti kuwa mtu mmoja amejeruhiwa. Uharibifu wa majengo kadhaa umeripotiwa pia katikati mwa mkoa wa Dnipropetrovsk na kusini mwa Odesa.