MigogoroUkraine
Urusi yafanya mashambulizi makubwa ya droni nchini Ukraine
27 Aprili 2025Matangazo
Gavana wa eneo la Dnipropetrovsk Serhiy Lysak, amesema mwanamume mmoja ameuawa katika mji wa Pavlohrad, huku msichana mwenye umri wa miaka 14 akijeruhiwa.
Pia ameongeza kuwa ng'ombe 500 waliuawa wakati droni ilipolenga eneo wanakofugwa.
Soma pia: Rais Trump akutana na Zelensky na kufanya mazungumzo
Kwa upande wake, jeshi la anga la Ukraine limesema kuwa limedungua droni 57 kati ya 149 huku nyingine 67 zikitoweka kwenye rada bila kufika shabaha zao, hali ambayo kwa kawaida hutokea kutokana na kuzuiwa na mifumo ya kielektroniki ya vita.