Urusi yafanya mashambulizi makubwa ya anga nchini Ukraine
29 Juni 2025Hayo yameelezwa leo na mamlaka za Ukraine zilizobaini kuwa aliyeuawa ni rubani wa ndege ya kivita chapa F-16. Yuriy Ihnat, mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha jeshi la anga la Ukraine, amesema shambulio hilo lilikuwa kubwa zaidi kwa kuwa Urusi ilitumia silaha za kurushwa kutokea angani zipatazo 537 ikiwemo droni 477 na makombora 60. Jeshi la Ukraine limesema limefanikiwa kudungua 249 huku zingine 226 zilipoteza mwelekeo.
Hayo yanajiri wakati siku ya Ijumaa, rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa tayari kwa awamu nyingine ya mazungumzo ya amani mjini Istanbul, lakini kuongezeka kwa mashambulizi hayo ya mabomu kunafifisha zaidi matumaini ya kufikia mafanikio katika juhudi za kuvimaliza vita hivyo vilivyodumu kwa miaka mitatu na kusababisha maafa makubwa.