MigogoroUlaya
Urusi yaendesha wimbi jipya la mashambulizi nchini Ukraine
10 Julai 2025Matangazo
Raia wanane wameuawa huko Donetsk na mmoja katika jimbo la Khmelnytsky huku wengine kadhaa wakiripotiwa kujeruhiwa huko Kyiv. Urusi imetangaza pia kuchukua udhibiti wa kijiji kingine cha mashariki mwa Ukraine cha Tolstoy.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ambaye Jumatano alikutana na Papa Leo XIV na mjumbe maalum wa Marekani Keith Kellogg mjini Roma, amewatolea wito washirika wake wa Magharibi kuzidisha vikwazo dhidi ya Urusi.